*Julai 7, 1954: Chama cha TANU kinazaliwa rasmi. Jina la TANU
lilitokana na wazo lililotolewa na Lameck Makaranga Bogohe, mmoja wa
waasisi wa chama hivho ambaye kwa sasa yuko chama cha UDP.
*Julai 7, 2008: Polisi mkoani Dodoma wanamkamata Kenneth Mdogo, makazi
wa kijiji cha Ilolo, wilayani Mpwapwa, kwa tuhuma za kumuua na kumtoa
macho Bibi yake wa kambo, Magreth Masinjisa (70) kwa imani za
ushirikina.
*Julai 7, 2005: Magaidi wanaushambulia mfumo wa usafiri wa treni chini
ya ardhi jijini London, Uingereza na kuua watu 56 huku 700
wakijeruhiwa.
*Julai 7, 1994: Mcheza sinema wa kike, Diane Lane aniomba mahakama
impe talaka dhidi ya mumewe, Christopher Lambert.
*Julai 7, 1994: Majeshi ya Yemen Kaskazini yanauvamia mji wa Aden.
*Julai 7, 1958: Rais Dwight Eisenhower wa Marekani anasaini sheria
inayoipa Alaska hadhi kamili kama jimbo la Marekani.
No comments:
Post a Comment