*Julai 8, 2008: Iddi Pandu Hassan, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar anatoa
ufafanuzi kuwa Zanzibar ni nchi lakina haina utaifa kwa sababu
iliusalimisha 1964 ilipoungana na iliyokuwa Tanganyika na kuwa sehemu
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
*Julai 8, 1923: Wakoloni wa Kiingereza Tanganyika wanapitisha Sheria
ya kikatili ya Kazi iitwayo Master and Native Servants Ordinance
ambayo inaweka adhabu ya mfanyakzi mwafrika anayetoroka kazini
kufungwagerezani au kufungwa kamba na kuburuzwa.
*Julai 8, 2008: William Ngeleja, Waziri wa Nishati na Madini,
analiambia Bunge kuwa Serikali imebaini kuwa imekuwa ikidhulumiwa kwa
kupipa gharama za ziada katika kampuni ya kuzalisha umeme ya IPTL.
*Julai 8, 2003: Ndege Namba 139 ya Shirika la ndege la Sudan inaanguka
na kuua abiria 116 karibu na mji wa Port Sudan.
*Julai 8, 1969: Marekani yaanza kondoa majeshi yake nchini Vietnam.
*Julai 8, 1982: Sophia Bush, mcheza sinema wa Marekani, anazaliwa.
*Julai 8, 1963: Marekani inapiga marufuku raia wa nchi yake kufanya
biashara yoyote inayohusisha fedha na nchi ya Cuba.
*Julai 8, 1919: Rais Woodrow Wilson wa Marekani anarudi nyumbani
kutokea Ulaya alikotoa mchango mkubwa katika makubaliano ya Mkataba wa
Amani wa Versailles, baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia.
No comments:
Post a Comment