Friday, February 24, 2012

JUNI 26 KATIKA HISTORIA (JUNE 26 HISTORY IN KISWAHILI)

Juni 26, 1995: Benjamin W. Mkapa, Waziri wa Sayansi, Teknolojia na
Elimu ya juu, anapitishwa na chama cha CCM kuwa mgombea Urais wa
Tanzania kupitia chama hicho tawala na kumshinda Jakaya Kikwete ambaye
katika uteuzi wa awali alikuwa ameiungwamkono kwa kura nyingi zaidi.
Juni 25, 1962: FRELIMO, Chama kilichopigania uhuru wa Msumbiji na
kuikomboa nchi hiyo kutoka ukoloni wa Wareno, kinaanzishwa jijini Dar
es Salaam na wakimbizi wa Msumbiji wanaoshi nchini.
*Juni 25, 1967: Mohammed Ali (Cassius Clay) anahukumiwa miaka mitan
jela baada ya kukaidi kujiunga na jeshi la Marekani wakati wa Vita vya
Vietnam.
*1941: Ujerumani chini ya dikteta Adolf Hitler unavamia Dubno, Poland
na kuwataka Wa-Ukrania wanaoishi hapo kuwafanyia lolote, ikiwa ni
pamoja na kuwaua, Wayahudi 12, 000 wanaoishi hapo.
*Juni 25, 1978: Hussein al-Ghasjmi, Raia wa Yemen Kaskazini, anauawa.
*Juni 25, 1994: Waziri Mkuu wa Japan, Tsutomu Hata, anajiuzulu.

No comments:

Post a Comment