Wednesday, February 22, 2012

AGOSTI 3 (MATUKIO MUHIMU YA KI-HISTORIA KATIKA TAREHE HII)

* Agosti 3, 1858: John Hanning Speke anakuwa mzungu wa kwanza kuliona
ziwa Nyanza na analiita ziwa hilo Victoria.
*Agosti 3, 1967: Marekani inapeleka wanajeshi 45, 000 kupigana na
jeshi la Vietnam huko Vietnam.
*Agosti 3, 1962: Lucky Dube, mwanamuziki maarufu wa Reggae anazaliwa
huko Afrika ya Kusini.
*Agosti 3, 1941: Martha Stewart, mwanamke maarufu sana Marekani katika
masuala ya uandaaji nyumba, jiko na vifaa vya ndani, anazaliwa.
*Agosti 3, 1984: Hisa 365.7 milioni zinauzwa katika soko la kimataifa
la hisa la New York, Marekani, ikiwa ni rekodi ya aina yake.
*Agosti 3, 1984: Watu 32 wanauawa katika bomu kwenye uwanja wa ndege
wa Madras, India.
*Agosti 3, 1985: Watu 35 anakufa katika ajali mbaya ya treni huko
Flaujac, Ufaransa.

No comments:

Post a Comment