*Agosti 4, 2004: Wahutu na Watutsi wanasaini mkataba wa amani Arusha, Tanzania.
*Agosti 4, 2009: Rais Mwai Kibaki wa Kenya anawasamehe wafungwa 4,000
wanaosubiri adhabu ya kifo na kuwapa kifungo cha maisha badala yake.
*Agosti 4, 1994: Lori lililkuwa limebeba mamilioni ya nyuki
linapinduka huko New York.
*Agosti 4, 1962: Wesley Snipes, mcheza sinema maarufu mweusi wa
Marekani, anazaliwa.
*Agosti 4, 1956: Meg Whitman, bilionea maarufu wa kike wa Marekani
aliyetajirika kupitia Ukurugenzi wa kampuni ya eBay, anazaliwa.
Anatajwa kuweza kuchukua U-Gavana wa jimbo la California baada ya
Arnold Schwarzenneger.
*Agosti 4, 1955: Billy Bob Thornton, mcheza sinema maarufu Marekani
aliyetamba zaidi katika filamu za Bad Santa na Sling Blade anazaliwa.
Aliwahi kuwa mwenzi wa muda mrefu wa mcheza sinema Angelina Jolie.
*Julai 4, 1988: Kampuni ya kukodisha magari ya Hertz inaamriwa kulipa
fidia ya dola milioni 23 za Marekani kwa kufanya biashara kwa
kuwarubuni wateja.
No comments:
Post a Comment