Agosti 5
*Agosti 5, 1905: Cassian Speiss, Askofu wa Kijerumani Tanganyika
anauawa na wazawa wakati wa Vita vya Maji Maji.
*Agosti 5, 1962: Patrick Ewing, mchezaji maarufu wa Mpira wa vikapu
katika ligi ya NBA Marekani, na baadaye kocha, anazaliwa.
*Agosti 5, 1997: Ndege ya Shirika la ndege la Korea aina ya Boeing 747
inaanguka ikiwa na abiria 331 huko Guam na abiria 29 tu wanasalimika.
*Agosti 5, 1997: Ramzi Yousef, gaidi aliyebuni na kufanikisha ulipuaji
bomu katika jengo la Kimataifa la Biashara Marekani, anafikishwa
mahakamani.
*Agosti 5, 1992: Askari wane wa Marekani wanafunguliwa mashtaka ya
jinai kutokana na kumpiga Mmarekani mweusi, Rodney King, kinyume cha
sheria. Kesi hii iliweka doa jeusi katika uhusiano wa weupe na weusi
Marekani.
*Agosti 5, 1994: Ndege aina ya Antonov-12 inaanguka huko Boda,
Siberia, iliyokuwa Urusi, na kuua watu 47.
No comments:
Post a Comment