Friday, February 24, 2012

JULAI 10 (JULY 12 HISTORY IN KISWAHILI) KATIKA HISTORIA

Julai 10
*Julai 10, 2008: Majambazi jijini Dare s salaam yanamvamia
mfanyabiashara Mwilima Kiomoni (65) wakati akiswali na kumkataisha
swala na kasha kumuua kwa kumpiga risasi kinywani ambayo inatokezea
kisogoni mwake kabla ya kumpora shilingi 75,00 na vito vya thamani
hukop Mbezi Msigani, Dare s Salaam. Yanafanya hivyo baada ya awali
kumdai atoe shilingiu milioni 8 ambazo hakuweza kuyapatia.
*Julai 10, 1967: JKT laanzishwa.
*Julai 10, 1982: Jessica Simpson, mwimbaji, mucheza sinema maarufu wa
Marekani anazaliwa huko Abilene, Texas. Ni mmoja wa nyota walioandikwa
na kutangazwa zaidi na vyombo vya habari huko Marekani.
*Julai 10, 1957: Cindy Sheehan, mwanaharakati maarufu wa Marekani na
mwanamke aliyepinga sera za Rais George W. Bush huko Iraq kuliko
mwanamke mwingine yeyote, anazaliwa.
*Julai 10, 1985: Jarida la Playboy linawashtua wasomaji na dunia nzima
baada ya kuchapisha katika ukurasa wake wa kwanza picha za aibu za
Madonna akiwa uchi wa mnyama.
*Julai 10, 1993: Melchior Ndadaye anakuwa Rais wa Kwanza wa Kihutu
nchinbi Brundi. Sylvie Kinigi,anakuwa Waziri Mkuu wake.
*Julai 10, 1964: Moise Tshombe anakuwa Rais wa Congo.
*Julai 10, 1991: Boris Yeltsin anaapishwa kuwa Rais wa Kwanza wa
Jamhuri ya Russia.
*Julai 10, 1978: Mapinduzi yasiyo na umwagaji damau yanafanyika nchini
Mauritania ambapo aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Moktar anaikimbia nchi.
*Julai 10, 1972: Kundi la tembo linakurupuka kutoka katika msitu wa
Chandika huko India na kuua watu 24.

No comments:

Post a Comment