Friday, February 24, 2012

JULAI 12 (JULY 12 HISTORY) KATIKA HISTORIA

*Julai 12, 1502: wakazi wa Kilwa wanakuwa Watanganyika wa kwanza
kabisa kulipa kodi nchini. Wanaanza kulipishwa kodi na wakoloni wa
Kireno.
*Julai 12, 1996: Sheria ya Usimamizi wa Ushindani wa Biashara inaanza
rasmi kazi kisheria. Sheria hii ilipitishwa na bunge kama sheria namba
4 ya 1994 na iko katika sura ya 285 ya sheria za nchi.
*Julai 12, 2008: Aliyekuwa Jaji Kiongozi Salum Massati, ambaye sasa ni
Jaji wa Mahakama ya Rufaa, anawapiga marufuku mahakimu na wahasibu wa
idara za mahakama kutumia vibaya pasipo maelezo fedha za mahakama au
kukopeshana fedha za maduhuli.
*Julai 12, 2006: Israeli inaishambulia Lebanon kulipiza kisasi kwa
askari wake kutekwa na wapiganaji wa Kiislamu wa Hezbollah.
*Julai 12, 1854: George Eastman, mvumbuzi wa kamera aina ya Kodak,
anazaliwa huko New York, Marekani.
*Julai 12, 1984: Geraldine Ferraro, anakuwa mwanamke wa kwanza kuwa
kugombea Umakamu wa Rais wa Marekani.
*Julai 12, 1996: Michael Jordan anasaini mkataba wa dola za Kimarekani
milioni 25 kucheza kwa mwaka mmoja katika ligi ya Taifa ya Mpira wa
vikapu ya Marekani.
*Julai 12, 1990: Boris Yeltsin anajiuzulu kutoka katika chama cha
Kikomunisti cha Urusi.
*Julai 12, 1817: Henry David Thoreau, mwandishi na mpigania amani,
anazaliwa huko Concord, Massachusetts

No comments:

Post a Comment