Wednesday, February 22, 2012

JULAI 18 (MATUKIO MUHIMU YA KI-HISTORIA KATIKA TAREHE HII)

*Julai 18, 1963: Tanzania inatangaza kufutwa kwa haki miliki zote za
ardhi zilizokuwa zimetolewa tangu ukoloni wa Uingereza kwa utaratibu
uitwao Freehold Titles (umiliki binafsi wa muda mrefu usio na ukomo wa
kawaida) na badala yake kubadlisha miliki zote za ardhi kuwa za
kupangiwa na serikali kwa kipindi cha muda fulani kama miaka 99 na
kadhalika (Government Leaseholds).
*Julai 18, 1536: Uingereza inakataa kuwa chini ya mamlaka ya Papa.
*Julai 18, 1932: Mkataba wa ushirikiano wa BENELUX unasainiwa kwa
pamoja na nchi za Ubelgiji, Uholanzi na na Luxembourg.
*Julai 18, 1995: Abiria wote 34 wanakufa katika ajali ya ndege aina ya
DC3 inapoanguka karibu na jiji la Antananarivo, Madagascar.
*Julai 18, 1992: Roger Ebert, mmoja wa wachambuzi wawili wa filamu
mahiri zaidi duniani anamuoa Chaz Hammel-Smith
*Julai 18, 1972: Rais Anwar Sadat wa Misri anawatimua wanajeshi 20,000
wa Urusi waliokuwa wakiisaidia nchi hiyo katika mafunzo na usalama.
*Julai 18, 1993: Rais Ishaq Khan wa Afghanistan na Waziri Mkuu wake,
Nawaz Sharif wanajiuzulu.
*Julai 18, 1977: Vietnam inakuwa mwanachama wa Umoa wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment