Friday, February 24, 2012

JULAI 5 KATIKA HISTORIA (JULY 6 HISTORY IN KISWAHILI)

JULAI 5
*Julai 5, 1980: Kesi ya mauaji ya raia katika mahabusu ya polisi
iliyoutingisha mji wa Mwanza inamalizika baada ya watuhumiwa wane
ambao ni maofisa waandamizi wa polisi kuhukumiwa kifungo cha miaka
saba jela kila mmoja na Jaji Nassor Mnzavas wa Mahakama Kuu Kanda ya
Mwanza ambaye anawatia hatiani kwa kumuua bila kukusudia Masanga
Mahula Mazegenuka mnamo Januari 1976. Wanaotiwa hatiani ni pamoja na
aliyekuwa Kamanda wa Polis wa Mkoa wa Mwanza, Isaias Kasian Mkwawa,
Askari Usalama wa Mkoa Godfrey James Ihuya, na wengine wawili.
*Julai 5, 1993: Watu 32 katika kijiji kimoja cha Uturuki wanauawa na
wanamgambo wa kabila la Kurd.
*Julai 5, 1985: Robert Mugabe anashinda uchaguzi Mkuu na Kuwa Waziri
Mkuu wa Zimbabwe. Zimbabwe ilipata uhuru mwaka 1980 na Mugabe
anaendelea kuongoza nchi hiyo hadi leo..
*Julai 5, 1973: “Live and Let Die” sinema maarufu ya James Bond,
inaonyeshwa kwa mara ya kwanza.
*Julai 5, Julai 5, 2003: Serena Williams anamshinda dada yake Venus
Williams katika fainali za mchezo wa tenisi za Wimbledon zinazotoa
bingwa anayeheshimika zaidi wa mchezo huo duniani.
*Julai 5, 1997: Martina Hingis amsmshinda Jana Novotna katika fainali
za Wimbledon (wanawake) na kuwa mchezaji bora zaidi wa tenisi wa

No comments:

Post a Comment